Jumapili, 25 Desemba 2016

NDEGE YAANGUKA BAHARINI URUSI

Kuna hofu kuwa huenda abiria wote 92 wamefariki baada ya ndege ya Urusi ya jeshi waliyokuwa wakisafiria kuanguka baharini katika eneo la black sea, Ndege hiyo ilipotea katika mitambo ya rada muda mfupi baada ya kupaa angani kutoka kwenye uwanja wa hoteli moja iliyoko maeneo ya black sea huko sochi. Ndege hiyo ilibeba abiria 91 wakiwemo wanajeshi wa urusi na kikosi cha bendi cha jeshi maarufu kwa jina la Alexandrov Ensemble.

Jumapili, 15 Mei 2016

HIFADHI ZETU

Tanzania ni nchi yenye vivutio vingi vya utalii, Mojawapo ni mbuga za wanyama, Ukiangalia katika hifadhi zetu za taifa utaona wanyama wa aina mbalimbali wakirandaranda humo,            Baadhi ya wanyama hao ni Twiga, Tembo, Pundamilia, Swala, Simba, Nyumbu na wengine wengi.             Nchi yetu imekuwa ikivutia watalii wengi kuja kuitembelea mara kwa mara na kuongeza pato la taifa katika sekta ya utalii,                         Ni vizuri na sisi wenyewe tukitembelea kwa utalii wa ndani ili kuongeza pato la taifa letu,                 Tazama hizi ni baadhi ya picha kidogo tu za wanyama waliopo kwenye hifadhi zetu za taifa

Hapo sokwe anakula matundaHuyu ni Tembo akiwa kwenye hifadhi huwa anapendeza sana muonekano wakeHawa pundamilia wapo sehemu mojawapo ya mbuga za wanyama mistari yao ya rangi nyeupe na nyeusi huonekana kama imechorwa na binaadamuHuyu ndege ni mmojawapo tu wa ndege ambao hupendelea kuishi kwenye hifadhi zetu za taifa pia inasemekana hupenda kula masalia ya nyama zilizoachwa na simbaKima hupendelea sehemu zenye miti iliyozibaTwiga ni wanyama wenye shingo ndefu ambazo husababisha kuwaona kwa urahisi hata ukiwa mbaliSimba wanaopanda kwenye miti pia hupatikana kwenye baadhi ya hifadhi zetuSimba huyu mkubwa akiwa kwenye mbuga za wanyamaTazama hawa simba wanavyo mrarua huyo nyumbu utaona ni jinsi gani simba walivyo na nguvuNyumbu pia wakati mwingine huwa na nguvu ya kumshinda simbaUkitembelea katika hifadhi za taifa utaweza kujionea na Nyati pia

Jumanne, 26 Aprili 2016

TUJITAHIDI NA MAZAO YA BIASHARA

Zao la Arizeti ni zao ambalo linahitaji mvua za wastani hata sehemu zenye ukame arizeti hustawi vizuri, Wakulima wengi wa zao hili wanakuwa na asilimia kubwa ya kufanikiwa kupata kuliko baadhi ya mazao mengine yanayohitaji mvua nyingi zao hili likiongezwa kulimwa kwa wingi litasaidia sana, tazama picha>>>

Jumamosi, 16 Aprili 2016

MISS TANZANIA 2014

Tujikumbushe kidogo, "Hizi ni picha za miss Tanzania mwaka 2014 LILLIAN KAMANZIMA katika muonekano wake