Jumanne, 28 Machi 2017

KUZAMA KWA FERI BANGLADESH

Watu watatu walikufa na wengine wengi hawajulikani walipo baada ya feri ambayo ilikuwa na msongamano kuzama mtoni katika wilaya ya Bagerhat nchini Bangladesh Jumaanne,                                                                         Afisa wa polisi alisema miili ya wanawake watatu imepatikana huku juhudi za kutafuta waathirika wengine zikiendelea.

( picha kwa hisani ya The Express Tribune )

Jumatatu, 20 Machi 2017

UBUNIFU

Mafundi hufanya ubunifu wa aina mbali mbali kuboresha kazi zao, Hapa tunaona mmoja wa mafundi wa kupiga rangi akiwa kazini tazama hiyo picha.>>> Fundi wa kupiga rangi aking'arisha moja ya dirisha ili lipendeze vizuri Hapa dirisha lililotengenezwa kwa ua la kipepeo limeshapigwa rangi ya kutu

Jumamosi, 18 Machi 2017

NDEGE ZAGONGANA NCHINI CANADA

Ndege mbili zimegongana zilipokuwa katika anga ya eneo moja la shughuli nyingi za kibiashara huko nchini Canada,     Rubani mmoja amefariki na mwingine kujeruhiwa vibaya sana, Polisi wanasema hata hivyo ni miujiza kwamba hakuna mtu mwingine yeyote aliye jeruhiwa licha ya ndege moja ya hizo kuanguka juu ya paa la mojawapo ya maduka makubwa ya eneo hilo nje kidogo mwa mji wa Montreal,  Ndege zote ni aina ya Cessnas kutoka shule moja ya urubani, Hali mbaya ya hewa inadhaniwa kusababisha ajali hiyo.