Jumapili, 25 Desemba 2016

NDEGE YAANGUKA BAHARINI URUSI

Kuna hofu kuwa huenda abiria wote 92 wamefariki baada ya ndege ya Urusi ya jeshi waliyokuwa wakisafiria kuanguka baharini katika eneo la black sea, Ndege hiyo ilipotea katika mitambo ya rada muda mfupi baada ya kupaa angani kutoka kwenye uwanja wa hoteli moja iliyoko maeneo ya black sea huko sochi. Ndege hiyo ilibeba abiria 91 wakiwemo wanajeshi wa urusi na kikosi cha bendi cha jeshi maarufu kwa jina la Alexandrov Ensemble.