Jumapili, 15 Mei 2016

HIFADHI ZETU

Tanzania ni nchi yenye vivutio vingi vya utalii, Mojawapo ni mbuga za wanyama, Ukiangalia katika hifadhi zetu za taifa utaona wanyama wa aina mbalimbali wakirandaranda humo,            Baadhi ya wanyama hao ni Twiga, Tembo, Pundamilia, Swala, Simba, Nyumbu na wengine wengi.             Nchi yetu imekuwa ikivutia watalii wengi kuja kuitembelea mara kwa mara na kuongeza pato la taifa katika sekta ya utalii,                         Ni vizuri na sisi wenyewe tukitembelea kwa utalii wa ndani ili kuongeza pato la taifa letu,                 Tazama hizi ni baadhi ya picha kidogo tu za wanyama waliopo kwenye hifadhi zetu za taifa

Hapo sokwe anakula matundaHuyu ni Tembo akiwa kwenye hifadhi huwa anapendeza sana muonekano wakeHawa pundamilia wapo sehemu mojawapo ya mbuga za wanyama mistari yao ya rangi nyeupe na nyeusi huonekana kama imechorwa na binaadamuHuyu ndege ni mmojawapo tu wa ndege ambao hupendelea kuishi kwenye hifadhi zetu za taifa pia inasemekana hupenda kula masalia ya nyama zilizoachwa na simbaKima hupendelea sehemu zenye miti iliyozibaTwiga ni wanyama wenye shingo ndefu ambazo husababisha kuwaona kwa urahisi hata ukiwa mbaliSimba wanaopanda kwenye miti pia hupatikana kwenye baadhi ya hifadhi zetuSimba huyu mkubwa akiwa kwenye mbuga za wanyamaTazama hawa simba wanavyo mrarua huyo nyumbu utaona ni jinsi gani simba walivyo na nguvuNyumbu pia wakati mwingine huwa na nguvu ya kumshinda simbaUkitembelea katika hifadhi za taifa utaweza kujionea na Nyati pia