Jumatatu, 6 Oktoba 2014

SALUM HASSANI MGAYA:

SALUM HASSANI MGAYA:Katika kutaja namba akakosea namba moja ya mwisho wakala akarusha pesa zikaenda kwa mtu mwingine, Kijana aliporudi tukakutana nikamuuliza mbona ujumbe wa pesa haujafika kwenye simu yangu akaniambia hajui kwa nini haujafika nikamuuliza jina lililotoka kwa wakala aliporusha pesa akanitajia jina tofauti na jina nililozoea lililopo kwenye akaunti yangu, Hapo nikasitisha shughuri zangu zote ikabidi tuende wote kwa wakala ili kama kuna uwezekano wa kurudisha pesa kutoka kwenye namba iliyokosewa atusaidie, Basi tulipofika tukamueleza wakala hali halisi iliotokea wakala akapiga simu makaomakuu na kuwaeleza kilichotokea nao wakaangalia zile pesa yule jamaa alikua hajatoa wakaizuia kutoa pesa ile namba, Sasa cha kushangaza ni kwamba kila tukienda kwa wakala anatuambia pesa bado ziko kwenye mtandao tumeyumba kwa muda wa wiki moja jibu likawa ni lilelile mwisho wake tukakata tamaa..<< MWISHO >>

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni