Jumamosi, 18 Machi 2017

NDEGE ZAGONGANA NCHINI CANADA

Ndege mbili zimegongana zilipokuwa katika anga ya eneo moja la shughuli nyingi za kibiashara huko nchini Canada,     Rubani mmoja amefariki na mwingine kujeruhiwa vibaya sana, Polisi wanasema hata hivyo ni miujiza kwamba hakuna mtu mwingine yeyote aliye jeruhiwa licha ya ndege moja ya hizo kuanguka juu ya paa la mojawapo ya maduka makubwa ya eneo hilo nje kidogo mwa mji wa Montreal,  Ndege zote ni aina ya Cessnas kutoka shule moja ya urubani, Hali mbaya ya hewa inadhaniwa kusababisha ajali hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni