Jumatano, 11 Januari 2017

MISITU YETU NI UHAI WA TAIFA

Kutunza misitu ni jukumu letu wote kwa ujumla, Tujitahidi kuilinda kwa namna tuwezavyo,   Tusipoilinda misitu yetu ya asili ambayo ni zawadi tuliyo tunukiwa na Mungu tutakaribisha jangwa na uhaba wa mvua utakao sababisha baa la njaa, Tukishirikiana pamoja tunaweza kuzuia uharibifu huu wa mazingira tunao uona ni mdogo kwa sasa lakini baadae athari zake ni kubwa, Tukiangalia uchomaji wa Mkaa ovyo ni chanzo kimojawapo cha uteketezaji wa misitu kwa haraka mno,   Tunalalamika sana kuhusu uhaba wa Mvua lakini tukitazama maeneo ambayo misitu bado ipo hakuna uhaba wa mvua ukilinganisha na maeneo ambayo misitu imeharibiwa kwa kiasi kikubwa, Asilimia kubwa ya kilimo chetu tunategemea mvua upungufu wa mvua unasababisha kipato kupungua sana na pia hata mazao yenye kustahimili ukame yatakosa nguvu kutokana na uhaba wa mvua,     Pia misitu ina faida nyingi sana tunaweza kufuga nyuki humo na tukapata Asali na tukaongeza kipato chetu, Na tukumbuke tunapo haribu misitu kuna Wanyama, Ndege, na Wadudu wa aina mbalimbali wanatoweka kutokana na uharibifu huu unaofanywa na binaadamu.   { Tutunze mazingira yatutunze } "Tazama baadhi ya picha"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni